Sunday, December 16, 2012

Swahili cultural items

Mchezo wa ng'ombe, Pemba (Bullfighting in Pemba)

Mchezo wa ng'ombe ni mmoja wa michezo ambayo inapendwa na Waswahili. Watu wengi hukusanyika mchezo huu unapochezwa. Mchezo huu huchezwa hasa Pemba.  Asili ya mchezo huu inasemekana ni Ureno. Tofauti na mchezo huu unavyochezwa huko Ureno, ng'ombe anaechezwa hauliwi. Ng'ombe hufungwa kamba ili iwe rahisi kumdhibiti asiwadhuru watu. Kabla ya ngombe kuachiwa uwanjani, hupigwa ngoma ambayo huwa na mpiga zumari. Watu wanaamini kuwa ng'ombe anaechezwa huwa na mashetani kichwani na ndio wanaomfanya ng'ombe huyo kuwa mkali.
Mtungi (water pot)

Huu ni mtungi. Ni chomba kinachotumiwa na Waswahili kwa ajili ya kuhifadhia maji ya kunywa. Mtungi hufinyangwa kwa udongo. Kwa kawaida mtungi huwekwa kipembeni. Pia katika utamaduni wa waswahili kila penye mtungi huweka pia kata. Kata ni chombo cha kunwea maji kutoka mtungini.Kata hutengenezwa kwa kifuu cha nazi na hutiwa mpini. Kata hufanana sana na upawa. Maji ya mtungi huwa baridi. Kwa kuwa mtungi upo katika utamaduni wa Waswahili kwa muda mrefu, ndio maana baadhi ya methali za Kiswahili zinautaja mtungi. Kwa mfano "siri ya mtu aijuae ni kata". Pia kuna msemo " ametulia kama maji ya mtungi"
Duka la wazila kuuzia kanga. Kanga ni vazi maarufu na muhimu kwa Waswahili hasa wanawake. Kanga kwa kawaida huwa na majina na wanaonunua, mbali ya kuangalia rangi, huangalia jina la kanga pia. aadhi ya watu hununua kanga kama zawadi kwa wake zao, wazazi wao au marafiki zao.


Nyumba ya bati. Mbele ya nyumba kuna mpapai.
Ngwachani, Pemba.


Makaa /Vipolo vya makaa
Kibanda cha kuku
Nyumba ya makuti
Nyumba ya udongo


Haya ni  makuti ya kuezekea nyumba hasa za udongo kama hiyo hapo juu. Makuti haya ambayo ni mabichi hukatwa kutoka kwenye mnazi. Makuti hayo hupasuliwa na baadae husukwa kama yanavyoonekana katika picha. Makuti hayo hufungwa juu ya paa la nyumba na hudumu kwa muda kidogo. Waswahili husema kuwa nyumba iliyoezekewa makuti hafanya watu walale usingizi mnono wakati wa mvua na hupunguza joto wakati wa kiangazi. Baada ya muda makuti yanapoanza kuvujisha, huezuliwa na huezekwa mengine. Pia kuna namna nyengine ya makuti ya kuwezekea ambayo huwa ni makavu na hayo husukwa tofauti na haya mabichi.
Kietezo
Shamba la muhogo
Choo cha makuti
Kanga
Down town Chake Chake,Pemba







1 comment: