Sunday, December 16, 2012

Food, Fruits and trees

Hizi ni mbirimbi (Averrhoa).
Mbirimbi huzaliwa kigogoni mwa mbirimbi. Mbirimbi hutumiwa kama kiungo cha mchuzi ili kuufanya mchuzi uwe mkali badala ya kutumia ndimu au limau. Mbirimbi pia hutumiwa kwa ajili ya kutengeneza achari. Mbirimbi hukatwa, na kutiwa chumvi na pilipili na baadae huanikwa juani. Baada ya mbirimbi kuiva, Waswahili hutumia mbirimbi wanapokula kama kitu cha kuleta ukali ukali katika chakula. Kuna utani kuwa watu wa Sebunyemi walihiyari ukatwe mkarafuu lakini mbirimbi(mti) usikatwe. Hiyo ni kuonesha ni kwa kiasi gani wanavyopenda mbirimbi.



Matufaa juu ya mtufaa


Banana tree
Mkungu wa ndizi juu ya mgomba. Hiyo inayoninginia inaitwa tojo. Majani ya mgomba hutumiwa kufunikiwa chakula kinapopikwa. Waswahili huyatumia majani hayo kwa matumizi mengine pia 


Hili ni Bungo
Bungo ni tunda maarufu miongoni kwa Waswahili. Waswahili hutumia  tunda hili kwa  ajili ya kukamua maji yake na kunywa. Unahitaji kutia sukari ili uweze kuona utamu wa maji ya bungo. Maji ya bungo (juisi) huwa rangi manjano.
Kombe
Makome

Maembe boribo
Sufuria juu ya iiko la mafya
Shelisheli la kuchemsha (boiled bread fruit)

Muhogo wa kuchemsha (boiled cassava)

Tufaa


                                                        Matufaa yakiwa juu ya mtufaa wake.

Matufaa (bellfruits) ni matunda ya kipekee ambayo yanapatikana visiwani Zanzibar na Pemba na maeneo mengine wanayokaa Waswahili. Matunda haya pia yanapatikana katika nchi za Malaysia, Indonesia na nchi nyengine za Asia. Baadhi ya watumiaji wa Kiswahili hawayajui matunda haya. Wasioyajua matunda haya huishia kuyaita maepul (apples) kuwa ndio matufaa. Hii si sahihi kwasababu matufaa ni matunda tofauti na maepul. Mti wa matufaa (mtufaa) ni jamii ya miti ya Myrtaceae. Mti unaozaa maepul uko katika jamii yamitiya Rosaceae.

Spice shop in Zanzibar.

Zanzibar island is well known for its spices. Many spices are grown in Zanzibar.  In the past  Zanzibaris would just grow spices for their daily use. People use spices (cardamom, ginger, cloves etc)  in their tea and also in their meat and rice. Spices are now a big business whereby people grow and harvest the spices and then pack them in small plastic bags as shown in the picture above and sell them to tourists. 

Zanzibar oranges and tangerines
Machungwa na machenza ya Zanzibar.

Hapa ni sokoni Zanzibar. Haya ni machungwa (upande wa kushoto) na machenza (upande wa kulia). Machungwa kwa kawaida huuzwa kwa mafungu. Fungu hilo hapo kwenye picha lina machungwa matano. Fungu moja la machenza pia lina nachenza matano. Upande wa kushoto mwa picha pia kuna mizani lakini machungwa hayapimwi. 
Fish in Zanzibar

Hapa ni soko la samaki Zanzibar. Samaki baada ya kuvuliwa na wavuvi huuzwa kwa wachuuzi na wao huwaleta hapa sokoni. Watu wanaohitaji kiteweo huja sokoni kununua samaki. Unaweza kununua samaki wa vipande au unaweza kununua wa mafungu au unaweza kununua samaki mzima. Kwa mfano, picha hii inaonesha samaki mmoja mkubwa anayeitwa Jodari (Tuna). Samaki huyu ana nyama nyingi.Kwa kawaida wachuuzi humkata vipande vipande na kumuuza. Samaki huyu nyama yake ni nyekundu. Pembeni mwa samaki huyo kuna fungu na ngisi (squid) . Na kwa upande mwengine kuna funga la samaki wa tasi. Hapa chini ni picha ya samaki hawa wa tasi wakiwa wameshapikwa kwa mchuzi wa nazi na kukamuliwa ndimu tayari kwa kuliwa. (the travelling pines)


No comments:

Post a Comment