Fishermen in local canoes in Pemba. |
Soko la Kengeja, Pemba. |
Mbele ya soko la Kengeja, Pemba. |
Hili ni tangi la maji.Tangi hili liko Kengeja, Pemba. |
Mchezo wa watoto (Children traditional play) Mchezo huu unaitwa "ana ana ano do". Jina la mchezo huu linatokana na nyimbo ya mchezo wenyewe. Ni mchezo maarufu kwa watoto wa Waswahili. Nyimbo yake inaimbwa hivi: "ana ana ana do, kachanika basto, ispiringi mitingo, ana kwa ana kadukuduku lembwe kafis" |
In this game, the children participating lay their hands face down whilst one child sings a song. The child who sings the song is also hopping from one hand to another with every syllable of the song. When the song stops, the hand the singer's finger rests upon is out. The process continues until the last hand remaining is the winner. |
Harusi ya Waswahili wa Zanzibar. (Swahili wedding in Zanzibar) Bwana harusi amevaa joho jeusi na kilemba. Mbele yake yuko shehe ambae ni muozeshaji. Shehe amevaa koti rangi ya dhahabu na amevaa kanzu na kofia. Pia mbele ya bwana harusi ni mtoa idhini kwa upande wa bibi harusi. Yeye humwambia shehe kuwa ametoa idhini kwa msichana kuolewa. Baadae shehe huenda kumuona bi harusi ili kuthibitisha kuwa amekubali kuolewa. Baada ya hapo shehe huozesha rasmi. |
Muslims graveyard. Hapa ni makaburini. Ni mahali panapochimbwa makaburi kwa ajili ya kuwazika Waislamu wanapofariki. Ukiangalia picha utaona wanaume watupu ndio waliopo makaburini. Katika utamaduni wa Waswahili, wanawake hawaendi makaburini. Kama aliekufa ni mwanamke, wanawake humuosha maiti na kumkafini na baadae hutiwa kwenye jeneza. Wanaume baadae humsalia na huenda kumzika. |
No comments:
Post a Comment